Pages - Menu

Monday, January 15, 2018

HATIMAE UMOJA WA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI YAADHIMIA KUSHIRIKIANA KUTAFUTA NJIA SAHIHI YA KUENDANA NA TEKNOLOJIA YA SARAFU DIGITALI NDANI YA MWAKA 2018.


Kutokana hali inayoendelea kwenye nchi za Afrika mashariki ya kushuka kwa uchumi na kuendelea kuporomoka kwa thamani ya sarafu zake,umoja  wa Benki za Afrika mashariki unaoundwa na nchi 6 zimefikia lengo la kuanzisha sarafu yake ya kidigitali itakayotumika kati ya nchi hizo 6, japokuwa hali ya ongezeko la watumiaji wa sarafu digitali nyingine kama Bitcoin kuendelea kukua kwa kasi, hii imeonekana kuwa changamoto kubwa na kizuizi cha nchi hizi kuanzisha sarafu yake (EAC currency),

Katika mkutano uliofanyika siku chache zilizopita mwaka huu nchi hizo zilikubaliana kuendelea kufatilia changamoto zinazoendelea kujitokeza kutokana na ongezeko la watumiaji wa sarafu hizo hasa Bitcoin na kupata majibu ya kitendawili cha kipi kitatokea endapo sarafu hiyo itaanzishwa angali wengi wanatumia sarafu nyingine.
Currency hii itaweza kutumika katika nchi za Burundi, Rwanda, Tanzania, Kenya, Uganda na Sudan ya kusini.
Mwezi December mwaka jana gavana mkuu wa benki ya Tanzania Mh. BENNO NDULU alikili kushuhudia mabadiliko makubwa ya kuzidi kuongezeka kwa wafanyabiashara wa sarafu hizi alipohojiwa na blog moja ya nje na kutamka kuwa
"Serikali inafahamu vyema kuhusu hili japo bado ni mapema sana kutoa maamuzi ila tupo kwenye mpango madhubuti wa kuendana na teknolojia hii na tamko rasmi ya kuziruhusu zitumike au zisitumike kisheria nchini litatoka hivi karibuni"
Mtandao wa Bitcoin.com ulijaribu tena kumtafuta ili ujue hitimisho lililofikiwa ambapo ulifanikiwa kuongea na kiongozi mkuu wa mfumo wa malipo ya kibenki nchini Tanzania na kusema kuwa
"Tanzania imeamua kushirikiana na nchi nyingine jirani ili kupata utatuzi wa suala hili japokuwa lengo la mvumbuzi wa Bitcoin lipo tofaut kidogo na like la umoja wa afrika mashariki hivyo tunategemea kupata changamoto nyingine, bado hadi sasa uchunguzi maalum unafanyika ili kujua changamoto hizo zitakazotokea na ndipo wazo kuu la kutengeneza sarafu digitali ya afrika mashariki litakapowekwa wazi"


Unahisi kuna faida yoyote ya kutengeneza sarafu digitali kwaajili ya afrika mashariki au no bora kuzikubali zilizopo na kuzitengenezea sheria itakayowalinda watumiaji?? Tuandikie mawazo yako katika nafasi wazi ya comment na kushare zaidi na wengine ili tupate mawazo chanya.

1 comment:

  1. Kiukweli hali ni nzuri endapo itaboreshwaa juu ya utekelezaji na usimamiz katika transaction.. piaa hata zile dust za transaction ndizo kidogo zinaleta wengee..ni ghali kidogo

    ReplyDelete