Nchi ya Venezuela imefungua usajili maalum utakaofungwa tarehe 20 January mwaka huu wa kuandikisha wataalam wote wenye ujuzi wa kuchimba sarafudigitali kama bitcoin ili kuweza kujadiliana na kuanza hatua za uchimbaji wa sarafu za nchi hiyo.
Kulingana na maelezo ya raisi yaliyorushwa na vyombo vya habari vya nchi hiyo hadi sasa idadi ya watu waaliojiandikisha imefikia 860,811. Sarafu hiyoinayoenda kutengenezwa kwa kunakili na kuifanyia marekebisho teknolojia iliyotumika kubuni bitcoin itaenda kufahamika kwa jina la PETRO.
Waziri mkuu wa mawasiliano nchini humo JORGE RODRIGUEZ aliviambia vituo vya habari nchini Venezuela kuwa wananchi wote wa VENEZUELA watawezeshwa kuzipata sarafu za PETRO na kuanza kuzitumia mara baada ya zoezi la kuzichimba kuanza, na wale wote watakaoshiriki katika zoezi hili la utengenezaji watapewa nafasi ya kutumia aina nyingine ya sarafu za kidigitali na usalama wa fedha zao kulindwa na serikali ya nchi hiyo kwa namna yoyoteilimradi tu ziwe ni zile serikali itakazopendekeza.
“Unahisi wananchi wa venezuela watakuwa tayari kuziacha kabisa sarafu nyingine na kuanza kuitumia PETRO pekee?”Andika maoni yako katika nafasi yacomment ya post hii…!!

No comments:
Post a Comment