Pages - Menu

Wednesday, January 17, 2018

BOBBY LEE ATABIRI MEMA KUHUSU CHINA NA SARAFU DIGITALI.

Kufuatiwa kuwepo kwa tetesi zinazosema kuwa serikali ya China imepanga kuzifungia kampuni zote zinazofanya biashara ya sarafu digitali nchini humo mara baada ya mwaka jana benki kuu ya nchi hiyo kuanzisha vikwazo juu ya kampuni zinazojishughulisha na uchimbaji wa sarafu digitali,, na ilianza kwa kutunga sheria ngumu zinazolenga kuzibana kampuni hizi.




Sheria hizi zilipelekea kampuni baadhi kufungwa kama RENMIMBI iliyokuwa ikifanya biashara zake nchini humo na nyingine kuanza kujiandaa kuhama kutafuta makao yake nchi nyingine.
Siku za hivi karibuni mwanzilishi na msimamizi mkuu wa kampuni ya BTCC ambae pia amejipatia ubilionea mkubwa kutokana na kufanya biashara hii ametabiri kuwa nchi nyingi kama China zitaonyesha kupinga teknolojia hii lakini mwishoni zitalazimika kukubali na kuendana nayo .
”Hamna mwananchi atakaelazimishwa kutumia kitu asichokipenda angali kizuri na bora zaidi kipo” BOBBY LEE alisikika akikiambia kituo cha habari cha CNN.
Ikiwa ni siku chache mara baada ya kauli ya Bobby Lee kutangazwa na vyombo vya habari hatimae serikali ya China imesikika pia ikisema haipangi kuikataa na kuitokomeza teknolojia hii bali kuichunguza na kuidhibiti kwa njia chanya dhidi ya matumizi makubwa ya nishati yanayotumika katika uchimbaji wa sarafu hizo.

Mmiliki wa kampuni nyingine ya uchimbaji wa bitcoin nchini humo (schwani) amesema mamlaka za kiserikali za nchi hiyo zimeagiza wachimbaji wote wa sarafu hizi kuwakilisha anwani zao pamoja na kiasi cha bitcoin wanazochimba kila siku. Sio huyo tu lakini pia mmiliki wa kampuni ya BITMAIN Wu Jihan alikiambia kituo cha habari cha Bishijie kuwa uchimbaji wa sarafu digitali kama bitcoin na matumizi yake kukua nchini humo zinaisaidia sana serikali ya nchi hiyo kuendelea hivyo sio rahisi kuitelekeza, Kinachotakiwa ni kutafuta njia mbadala dhidi ya matumizi makubwa ya nishati yanayotumika.


Nini maoni yako juu ya utabiri wa Bilionea Bobby Lee?

No comments:

Post a Comment