Mnamo january
3 2009 bitcoin(sarafu digitali) ya kwanza iligunduliwa na mtaalamu wa kuunda
programu mbalimbali za kompyuta na masuala ya kiuchumi aitwae SATOSHI NAKAMOTO.
Kabla Satoshi
Nakamoto kutoweka kusikojulikana aliweka utambulisho wake wazi akijitaja kama
raia wa wa japani mwenye umri wa takribani miaka 37. Utambulisho unaonekana kuwa
sio sahihi kulingana na uwezo wake wa kuandika lugha ya kingereza kwa ufasaha
na katika kuunda program iliyotumika kutengeneza bitcoin na tovuti ya
bitcoin.org
Aliendelea
kusaidiana na kundi lake hadi katikati ya mwaka 2010 ambapo alikabidhi kila
kitu kwa GAVIN ANDRESEN (mwanzilishi wa 3D graphics na mtaalam wa programu za
virtual reality) baada ya kukamilisha zoezi zima la uundaji wa bitcoin.
Hadi sasa
hamna ukweli halisia unaomtambulisha Satoshi Nakamoto japokuwa yapo makisio
mbalimbali yaliyopatikana kumuhusu mtafiti ma mtaalamu huyu aliyeleta mapinduzi
makubwa katika sekta ya fedha na teknolojia duniani kote.
Yapo makisio
yanayosema haikuwa mtu mmoja bali kundi la watu wenye dhamira moja, lakini pia
ukweli huu sio halisia kwa sababu ya kukosa vithibitisho kamili.
Bitcoin kwa
lugha rahisi tunaitafsiri kama sarafu digitali inatengenezwa kwa mchakato
uitwao mining na kumbukumbu zake huifadhiwa kwenye
mfumo maalumu uitwao blockchain ambao pia hutumika katika uhamishaji wa bitcoin
kutoka kwa mtumaji X kwenda kwa mpokeaji Y bila kuwepo kwa mamlaka yoyote ya
kifedha katikati,.
Neno Mining
katika utengenezwaji wa bitcoin halina maana ya uchimbaji wa madini kama
ilivyozoeleka bali lina maana ya mchakato wa kutatua mantiki za kihesabu kwa
kutumia program maalum za kompyuta.Mara baada ya mchakato huo kukamilika
makundi ya bitcoin yanayopatikana(block) huwekwa katika mfuatano/mlolongo maalumu(chain)
kulingana na jinsi yalivyopatikana na ndio maana hutambulika kama blockchain.
Kadri bitcoin
zinavyotengenezwa ndivyo mfuatano/mlolongo huu huongezeka urefu na ugumu pia
katika utatuzi wa mantiki za kihesabu pia huongezeka. Hii imepelekea thamani yake
kihesabu kupanda lakini pia gharama za uhamishaji(transaction fee). Changamoto
hii imeweza kutatuliwa na baadhi ya sarafu digitali nyingine zilizovumbuliwa
baada ya bitcoin ni kama Ethereum.
MAENDELEO YA BITCOIN TANGU KUUNDWA
KWAKE.
Japokuwa
sekta nyingi za kifedha duniani zimeonyesha kuvutiwa na mapinduzi haya ya
kiteknolojia bado zina mashaka kuhusu utekelezaji wa utumiaji wa sarafu za aina
hii. Mnamo mwaka 2014 tulishuhudia benki kuu ya Australia ikifunga akanti zote
zilizotumika katika ununuaji au uuzaji wa bitcoin.Kati ya miaka ya 2013 na 2014
mamlaka kuu ya benki za ulaya na mamlaka ya udhibiti wa taasisi za kifedha
nchini humo zikitoa tahadhari kuhusu hatari iliyopo katika uwekezaji wa sarafu
hii ya bitcoin uliokuwa ukiendelea.
Ndani ya
mwaka huo wa 2013 pia Forbes ilitaja uwekezaji katika bitcoin kama uwekezaji
bora wa mwaka huo wakati ilipofika 2014 kituo kikubwa cha habari cha Blomberg
kiliutaja uwekezaji katika bitcoin kama uwekezaji mbaya kuliko uwekezaji wowote
duniani.
Ilipofika
2015 meza ya habari ya kituo cha Blomberg ilishuhudia kufunikwa kwa habari
zilizohusu bitcoin tu katika upande wa habari za kifedha na kiuchumi kwa
ujumla.
Kwa mujibu wa
bitincharts.com (tovuti inayoonyesha ukuaji wa bitcoin) hadi kufikia mwaka 2017
kulikuwa na bitcoin wallet(mifuko maalumu ya kimtandao inayotumika kuhifadhi
bitcoin) ipatayo 9,272 yenye bitcoin zenye thamani zaidi ya dola za kimarekani
million 1.
Wapo pia
mabepari kama Peter Thiel ambao waliwekeza zaidi ya dola za kimarekani milioni
3 ili kusaidia miradi na sekta mbalimbali zilizohusika na maendeleo ya sarafu
hii.
VIDEO IKIELEZEA NAMNA BITCOIN INAVYOWEZA KUONDOA UMASIKINI DUNIANI.
ASILI YA BITCOIN KUWA NA BEI TETE.
Mnamo mwaka
2011 bei ya bitcoin ilikua ghafla na kufikia dola 30 za kimarekani (takribani
67,200/=). Badae katikati ya mwaka 2013 na 2014 tarehe 10 mwezi aprili bei ya bitcoin ilikua
zaidi na kufikia dola 266 za kimarekani (takribani 595,840/=) kabla ya kuanguka
tena thamani yake hadi dola za kimarekani 50(takribani 112,000/=)
Hadi kufikia
mwezi august mwaka 2014 bei ya bitcoin ilikuwa chini ya dolla
600$(1,344,000/=).Kulingana na maelezo ya gwiji wa mambo ya kiuchumi Mark T
Wiliam, bitcoin ina hali ya kuwa na bei tete mara 7 zaidi ya bei ya dhahabu.
Ndani ya
mwaka 2013 waandisi wa habari, wanachumi na benki kuu ya Estonia walipaza sauti
wakiitaja sarafu ya bitcoin kama mpango wa kimtandao ulioundwa ili kutapeli
watu na haikuwa biashara wala sarafu halisi. Mwanasheria profesa wa sheria
katika chuo cha chikago alisimama kuthibithisha kuwa bitcoin haikuonekana kuwa
mpango danganyifu sababu hakipo ata kimoja kilchosemwa kuhusu bitcoin ambacho
kilionekana kuwa uongo, watu waliweza kuimiliki katika mifuko yao ya kimtandao,
kuuza na kununua bila taasisi zozote za kifedha za kati kuhusika, bei pia
ilipanda na kushuka kulingana na mahitaji yake, yote hayo yalikuwa halisi, yalioonekana
na haikuwa udanganyifu.
Mwishoni wa
mwaka 2014 benki kuu ya dunia ilithibitisha na kuhitimisha kuwa bitcoin haikuwa
mpango danganyifu bali kitu halisia. Sio benki kuu ya dunia tu, Shirikisho la
balaza la fedha la uswisi lilihitimisha pia kwa kusema bitcoin haikuwa mpango
danganyifu sababu kulikuwa hamna faida yoyote iliyohaidiwa katika uwekezaji
wake bali makisio ya mtu binafsi na kupenda kujihusisha katika uwekezaji wake.
Adi mwezi
julai mwaka 2017 sekta na taasisi nyingi za kifedha dunia tayari zilikuwa
zimeikubali bitcoin kama sarafu halisia na sio mpango danganyifu isipokuwa
baadhi ya watu binafsi maarufu kama bilionea na mwekezaji maarufu aitwae Howard
Marks ambae bado aliendelea kuitaja bitcoin kama mpango danganyifu. Tarehe 12 mwezi
Septemba, Jamie Dimon (Mmoja kati ya watendaji wakuu wachache sana duniani kuwa
mabilionea) ambae alikuwa akitumikia kama mkurugenzi mtendaji wa moja kati ya
benki kubwa duniani inayotajwa kuwa ya sita kwa kumiliki mali zenye thamani
kubwa duniani iitwayo JP Morgan Chase, aliitaja bitcoin kama udanganyifu wa
kimtandao na alitoa onyo kali katika kampuni yake kwa yoyote ambae
angejihusisha na biashara ya bitcoin angepoteza kazi yake. Zero Hedge (tovuti
inayotoa habari za kiuchumi) ilitoa fununu kuwa wakati Howard Dimon akitoa onyo
hilo JP Morgan mwenyewe alitajwa akinunua bitcoin kwaajili ya wateja wake. Tarehe
9 mwezi january 2018 Jamie Dimon ameonekana akiongea na shirika la habari la CNN
akisema anajutia kuiita biashara hii ya bitcoin kama biashara danganyifu ambapo
thamani ya bitcoin moja imefikia kiasi cha kuuzwa takribani dola za kimarekani
14,398 (kati ya 35,521,281/= na
46,461,909/=)
Kutokana na
ongezeko la bei ya bitcoin siku hadi siku mabilionea wengi sana ambao walinunua
wakati ikiwa chini wameendelea kuonekana kona nyingi za dunia.
………………………….
Tutaendelea katika post ijayo kuwataja mabilionea
ambao wamebadilisha kazi zao na kujikita katika biashara hii ya sarafu za
kidigitali, benki za nchi mbali mbali ambazo zimeikubali bitcoin na matarajio
makubwa yaliyopo yaliyopo katika sarafu hizi kwa wawekezaji wake. Ahsante!!

No comments:
Post a Comment