KENYA NA AFRIKA YA MASHARIKI
Kenya ilijulikana kupitia Bitpesa (Tovutia
inayoweza mteja kubadili bitcoin kuwa fedha na fedha kwa bitcoin) ambayo
imesaidia nchi za afrika ya mashariki kuitumia sarafu ya bitcoin kwa
kasi
zaidi.
Lakini pia mtandao wa mawasiliano wa
M-PESA mwaka 2017 ulisikika ukisema
“tunaona fursa kubwa ndani ya bitcoin na teknolojia hii mpya".
NIGERIA
Hii ni kati ya nchi zenye idadi kubwa
ya watu barani Afrika na inachukuliwa kama nchi mojawapo inayoikubali na
kuitumia bitcoin kwa kiasi kikubwa. Haikuwa maajabu ilipofika oktoba 2016
Bitx (Tovuti inayojishughulisha na uhifadhi wa bitcoin) ilipofikisha
mipakuo(downloads) takribani 100,000 kutoka nchini humo pekee.Ilipofika mwezi
Julai mwaka 2017 kiasi cha fedha iliyopo kwenye mzunguko LocalBitcoin (Tovuti
nyingine inayosaidia uuzaji na ununuaji wa bitcoin) ilipofika dola za
kimarekani milion 3, na kati ya hizo asilimia 32 ilikuwa ikitoka nchini
Nigeria.
Benki kuu ya Nigeria imeendelea
kusema bado inafatilia njia chanya ya
kuendana na mabadiliko haya ya kiteknolojia.
AFRIKA KUSINI
Mfuko wa kuhifadhi bitcoin wa BITX
adi kufikia 2017 ilikuwa imefikisha asilimia 66 ya watumiaji kutoka Afrika
kusini, wakati 23 kati ya hao walikuwa wakiitumia sarafu hii kwenye uhamishaji
wa fedha wa haraka, na asilimia 40 wakiitumia kama sehemu ya uwekezaji. Lakini
pia hadi sasa Afrika kusini ni kati ya nchi zinazomiliki ATM ya huduma za
BITCOIN.
GHANA NA AFRIKA YA MAGHARIBI
Tovuti ya Ghana Dot Com imesaidia
sana katika kuifanikisha teknolojia hii kufika mbali baada ya kuanzisha
mchakato wa kutengeneza bitcoin nchini humo chini ya uongozi wa profesa NII
NARKU QUAVOUR, ambapo kwa hesabu inachangia asilimia 3 ya ada zote kwenye mfumo
wa blockchain (blockchain fees).
Tovuti nyiingine ijulikanayo kwa jina
la KITIWA, Mwezi Juni ilifikisha takribani dola za kimarekani 40000 kutokana na
kuunganishwa na kampuni nyingine ya mawasiliano na simu za mkononi KITIWA ilionyesha kufikia
viwango vya juu zaidi vya ubora katika kuendeleza huduma hii.
ZIMBABWE
Ilipofika mwaka 2017,Bitcoin ilivunja
rekodi kwa mara ya kwanza duniani kote kwa kufikisha bei ya dola za kimarekani
2000 (takriban 4,800,000/=) nchini ZIMBABWE. Baada ya benki nyingi za ZIMBABWE
kukumbwa na vikwazo vingi kutokana na migogoro ya kisisasa uliyokuwa ikiendelea
nchini humo.
Ziliona teknolojia ya bitcoin kama njia
mbadala na fursa pekee ya kuziendeleza kutokana na asili ya bitcoin ya
kutofungamana na sekta za kifedha za kiserikali.
Shukrani kwa LocalBitcoin (Tovuti ya
kuuzia na kununulia bitcoin iliyopo nchini zimbabwe) iliyosaidia sana biashara
hii, ambayo ilishuhudia ongezeko kubwa la watu kutoka zimbabwe na kuifanya
kufungua matawi mawili zaidi yafahamikayo kama BitMari na BitFinance.
Sio hivyo tu, watu wameendelea
kuiamini bitcoin hadi kufikia kuitumia kwenye matumizi ya kawaida kabisa kama
vile kutolea mahari, inaweza kuwa kitu cha ajabu lakin kijana mmoja afahamikaye
kwa jina la ANTONY MBURU alionesha kuiamini zaidi sarafu hii na kuitumia kulipia
mahali mara baada ya kuongezeka zaidi ya mara 10 tangu alipozinunua, kituo cha
habari cha NTV kilimuonyeha akisema.
Matukio mengi kuihusu bitcoin
yameendelea kutokea nchini humo siku hadi siku.
Nchi nyingine ambazo wananchi wake
wametajwa wakionyesha kushiriki sana katika biashara hii ni Uganda na Tanzania,
Nchi ya SENEGAL imetoa kauli rasmi ya kuanza kuitumia teknolojia hii mwishoni
mwa mwaka huu na kuisambaza kupitia WESTERN AFRICA AND MONETARY UNION.
No comments:
Post a Comment