Kulingana na sarafu hii kuendelea kuvutia wawekezaji
wengi kutokana na lengo lake la kurahisisha mahamisho ya kifedha kwenye
mashirika ya kibenki mbalimbali kwa gharama nafuu na haraka, tayari benki kama
standard chartered na nyingine nyingi kubwa zipo mbioni kuanza kuitumia,
hii imepelekea idadi ya wawekezaji kuongezeka kadri siku zinavyokwenda.
Sarafu digitali nyingi zimejaribu kushindana na Bitcoin
ila ziliishia katikati na bado Bitcoin iliendelea kuonyesha uimara wake,
Tumeshuhudia kwa siku kadhaa kuwa ilikuwa rahisi sana kwa sarafu digitali
nyingi zikizopo nje ya 5 bora katika soko la fedha za kidigitali kuongezeka
thamani hadi mara 3 kwenye kipindi cha wiki tu ila bado haikuwa rahisi kuipita
Bitcoin.
Bitcoin imetengeneza record nyingi za kupanda hadi
asimilia 14 ndani ya masaa 24 ambapo record hii imevunjwa na ripple mara kadhaa
kwa kupanda hadi asilimia 16 ndani ya masaa 24 tu. Hadi sasa ripple imefikisha
takribani dola za kimarekani bilioni 104 ambapo Bitcoin inakadiliwa kuwa dola
bilioni 245 katika soko la sarafu hizi.Endapo ripple itaongezeka na kufikia
dola 6.75 wakati bei ya Bitcoin ikibaki ilivyo sasa, Ripple itachukua namba
moja na kuhesabiwa kama sarafu namba moja kwenye soko la sarafu digitali
kutokana na idadi kubwa ya sarafu hizo ukilinganisha na Bitcoin.
Soko la sarafu hizi limeendelea kuwa gumzo na kitendawili
kwa wengi hata kwa wale wazoefu kwenye sekta za kifedha, wapo matajiri ambao ni
mfano kwa wengi ambao husikika wakizitaja vibaya sarafu hizi na kisha kuonekana
wakiwekeza kiwango kikubwa cha fedha siku chache baadae, pengine hata masaa
machache baadae baada ya sarafu kushuka thamani. Huu ni mchezo ambao umetajwa
na tovuti nyingi za sarafu digitali kufanyika sana hasa ndani ya mwaka 2017.
Zimekiri kwa kusema kuwa tunaweza kusema ukweli mmoja tu
kwa sasa kuwa sarafu digitali hazina njia ya kuepukwa hivyo in lazima kila mtu
atazitafuta, wenye upeo wameliona hilo ndio maana baadhi hutumia nguvu zao na
imani iliyopo kwa watu wao kuongea vibaya kuhusu teknolojia hii ili thamani
yake ishuke walau kwa asilimia kadhaa na kisha kuwekeza kiasi kingi ili siku za
mbeleni ukazitafute kwao" tovuti kama Bitcoin.com ilidai hivyo.
Wapo matajiri walioweka wazi kuwa
"sio wazo baya mtu kuwekeza walau asilimia 10 ya kipato chake anachoweza kuingiza kwa mwaka mzima kwenye sarafu hizi, japo ni vyema mtu kutumia muda wa kutosha kuifatilia kisha kufanya maamuzi binafsi."
Unahisi ni rahisi teknolojia hii kupita na kutokomea
kabisa na kuturudisha katika utumiaji wa sarafu za kawaida kama baadhi
wanavyohisi au ni kauli tu zinazotumiwa na mabepari kukatisha tamaa na wao
wawekeze kwaajili ya manufaa ya baadae!?
Unaweza kutoa maoni yako katika nafasi ya comment na kushare mawazo yako kwa pamoja !

No comments:
Post a Comment