Pages - Menu

Monday, January 15, 2018

HATIMAE NJIA MPYA YA KULINDA USALAMA WA WAWEKEZAJI KATIKA SARAFU DIGITALI YAPATIKANA NCHINI GIBRALTAR....!


Sheria iliyopitishwa tarehe 1 January mwaka huu nchini Gibraltar inayozitaka kampuni zote zinazojihusisha na sarafu digitali hasa Bitcoin kuwa na leseni maalum za kiserikali kutoka mamlaka ya GFSC (Gibraltar Financial Service Commission).
The chief Minister of Gibraltar
Hon. Fabian Picardo



Sheria hii inazitaka kampuni hizo kuboresha njia za mawasiliano kati yao na wateja na kutunga sheria binafsi za kila kampuni zinazolenga kulinda masilahi ya fedha zinazowekwa na wananchi katika biashara hiyo,sheria hizo zitapitiwa na mamlaka hiyo kwa umakini kabla ya kutumika.
Mwezi December mwaka jana bunge la nchi hiyo liliadhimia na kuweka wazi lengo lake la kuhakikisha Gibraltar inakuwa nchi pekee yenye mvuto wa uwekezaji katika biashara hiyo na utumiaji mzuri wa teknolojia hii.

Serikali ya nchi hiyo hadi sasa inaonyesha kwa kiwango kikubwa kuiamini teknolojia hii mpya ya sarafu za kigeni na kuitumia kama njia ya kurudisha uchumi wake katika hali ya kawaida Mara ya baada ya uchumi wao kuyumbishwa na kuharibika kwa British naval dockyard (bandari kubwa iliyokuwa ikitegemewa na nchi ya Gibraltar.)

No comments:

Post a Comment