Nchi ya Venezuela imefungua usajili maalum utakaofungwa tarehe 20 January mwaka huu wa kuandikisha wataalam wote wenye ujuzi wa kuchimba sarafudigitali kama bitcoin ili kuweza kujadiliana na kuanza hatua za uchimbaji wa sarafu za nchi hiyo.
Kulingana na maelezo ya raisi yaliyorushwa na vyombo vya habari vya nchi hiyo hadi sasa idadi ya watu waaliojiandikisha imefikia 860,811. Sarafu hiyoinayoenda kutengenezwa kwa kunakili na kuifanyia marekebisho teknolojia iliyotumika kubuni bitcoin itaenda kufahamika kwa jina la PETRO.






