Baada ya kushuhudia gharama za
mahamisho ya bitcoin yakipanda kwenye robo ya mwisho mwaka 2017, hatimaye
zimeanza kushuka kwa mara nyingine. Leo tovuti ya Bitcoinfee.com imeonyesha
wastani wa dola 15 kwa kila mahamisho ya bitcoin yaliyofanywa duniani.
Tovuti za kubadilisha bitcoin kama
bitfinex, wiki hii imetangaza pia kutakuwa na kupungua kwa kiasi kikukwa kwa
gharama za kutoa bitcoin kutoka kwa watumiaji wa tovuti hii.
Japokuwa wastani wa gharama za
mahamisho ya bitcoin ya dola 14 mpaka dola 16 bado kuonekana zipo juu ila haya
ni maendeleo makubwa ukilinganisha na wastani wa dola 30 iliyokuepo mwaka jana
mwezi December.
Masaa machache yaliyopita tovuti
nyingine za localbitcoin pamoja na BTC.com
zimeongeza teknolojia ya segwit inayolenga kupunguza gharama za
mahamisho ya bitcoin na hiyo imeshuhudiwa na watumiaji wake wengi baada ya
gharama kupungua. BTC.com iliongeza kwa kuandika katika blog yake kuwa
"watumiaji wake watafurahia huduma yake kutokana na kushuka kwa gharama. Hii imetokana na teknolojia ya segwit kuongezwa katika mifumo yake ya mifuko ya kuhifadhia bitcoin kwa watumiaji wote wa simu za mkononi na kompuya''.
Hadi sasa ni asilimia 11 pekee ya
kampuni zinazojishughulisha na bitcoin zilizoikubali teknolojia ya segwit yenye
lengo la kupunguza gharama, pengine matokeo haya ya kupungua kwa gharama za
uhamishaji wa bitcoin yanayoendelea kuoneshwa na kampuni zinazoitumia
teknolojia hiyo zitapelekea kampuni nyingi kuitumia.
Unahisi nini athari na faida za kuitumia teknolojia hii katika matumizi ya bitcoin? toa maoni yako katika nafasi ya comments iliyopo chini.

No comments:
Post a Comment