Mapacha hawa
walizaliwa mnamo tarehe 21 mwezi August 1981, wajasiliamali wakubwa wa biashara
za internet (internet). Umaarufu wao ulianza mwaka 2014 mara baada ya
kumshitaki Mark Zuckerberg (mmiliki wa mtandao wa kijamii wa facebook) madai ya
kuwa aliiba wazo lao la mtandao wa kijamii unaounganisha watu. Walishinda kesi
hiyo na kulipwa takribani dola milion 65 za kimarekani (takribani sh 139,750,000,000/= za kitanzania).
Mapacha hao
Cameron na Tyler winklevoss walitumia fedha hizo kuwekeza katika bitcoin.
Walikiambia kituo cha habari cha CNBC kwa kuwa walijiingiza katika bitcoin na
kuanza kuifatilia tangu mwaka 2012 wakati bitcoin ikiwa na thamani ya dola za
kimarekani 10(takribani 22,400/= za kitanzania)
Hadi kufikia
leo utajiri wao umeongezeka ma kufikia dola bilioni 1.3
WINK LEVOSS MAPACHA MABILIONEA WA KWANZA WA BITCOIN
Huyu ni
mwanzilishi wa Shirika la Microsoft, Mfanyabiashara wa kiamerika na mwekezaji
mkubwa. Hadi kufikia January mwaka 2018 utajiri wake umeongezeka na kufikia
dola za kimarekani bilion 91.1 kutoka dola za kimarekani bilioni 84.4 mwaka
2014 alipowekeza katika bitcoin. Billgate aliwekeza asilimia 0.5 tu ya utajiri
wake wa wakati huo. Billgate amesikika mara nyingi akisema “Njia halisi ya kuwa
bilionea bila kuwa na asilimia kubwa za kupoteza mtaji wakoni kuchunguza dunia
inapoelekea na kufika huko wa kwanza kwa kuwekeza”
Mwaka 2014
alikiambia kituo cha BLOOMBERG kuwa Bitcoin ni zaidi ya sarafu na inaleta mvuto
zaidi na ushawishi kuitumia katika mahamisho makubwa ya kifedha”
Utafiti
unasema kwamba kama WINKLEVOSS BROTHERS wanamiliki zaidi ya Bitcoin 100,000 ni
rahisi kwa mtu kama Billgate kumiliki chache zaidi ya hizo. Ukilinganisha
thamani ya bitcoin 100,000 ilikuwa ni sawa na dola za kimarekani milioni 45, hiyo
ilikuwa ni chini ya asilimia 0.5 ya utajiri wa Billgate kwa wakati huo. Alisikika
akisema kuwa Bitcoin bado ipo hatua za mwanzo sana na ni rahisi kumfanya mtu
yoyote trilionea.
Alizaliwa
mnamo tarehe 14 May mwaka 1984, ni mtaalamu wa kutengeneza program za kompyuta
na mjasiliamali mkubwa wa biashara za kimtandao. Hadi kufikia Nov mwaka 2017
alikuwa akikadiliwa kuwa na utajiri wa dola za kimarekani milion 74.2
Taarifa
zilizotoka January 5 mwaka huu zinasema Mark Zuckerberg ameweka wazi kuhusu
mpango wake kwenye mabadiliko haya ya kiteknolojia na alishaanza rasmi
kuangalia jinsi ya kufanya uwekezaji zaidi katika teknolojia hii ya sarafu za
kidigitali kama bitcoin wakati akiongea na kituo cha habari cha CNBC. Hadi sasa
yupo kwenye hatua za kuifahamu kiundani.
Alipokuwa na
miaka 15 aliwaomba sana wazazi wake kuwa angependa aachane na shule sababu ya
mwalim mmoja aliyekuwa akimsumbua college. Alianza kumchukia mwalimu huyo baada
ya kumkaripia kwa kumwambia kuwa hakuwa kitu ni bora aachane na shule na
akaajiliwe katika kiwanda cha kuoka mikate na keki cha Mc Donalds. Ndipo Finman
alipoamua kuweka DAU na wazazi wake kuwa endapo atafikisha miaka 18 akiwa
milionea basi wasingemlazimisha tena kuendelea na shule. Alisikika pia akisema
katika kituo kimoja cha habari kuwa “Naushukuru uwekezaji wangu wa utani na
hasira katika bitcoin, sitalazimishwa tena kuendelea na masomo”.
Hadi sasa
Finmani anamiliki takribani bitcoin 403 ambazo zina thamani ya kila moja na
kuufikisha utajiri wake kiasi cha dola za kimarekani milioni 1. Amewekeza pia
katika sarafu nyingine za kidigitali kama litecoin na Etheleum.
Finman
alisema “Siku njema zitaendelea kuja na thamani ya sarafu za kidijitali
tukizishuhudia zikipanda hadi mara 1000 zaidi ya zilivyo sasa”
Finman
alianza kwa kuwekeza dola 1000 (takribani 2,240,000/=) mwaka 2011 alipokuwa na
miaka 12, zawadi aliyopewa na bibi yake na kaka yake Scott.
Kijana mwenye
umri wa miaka 24 anaesemekana kuwa kijana mwenye bahati sana kuwahi kutokea
baada ya kuwekeza katika bitcoin.
Mnamo mwaka
2013 rafiki yake alimpa zawadi ya bitcoin ili wabadilishane kwa fedha ndogo
sana. Alizoea kuona watu wakiitumia kununulia vitu vidogo sana kama pizza
wakati huo.
Ilipofika
mwaka 2017 Gardner alipatwa na bumbuwazi wakati akiwa matembezini nchinin
afrika ya kusini. Aliingia mtandaoni baada ya kusikia fununu na kukuta thamani
ya bitcoin moja kupanda na kufikia dola za kimarekani 2400 (takribani
40,057,243/=). Anaitabili bei ya bitcoin kuendellea kupanda zaidi na kufikia
kiasi cha kuweza kumilikiwa na watu wachache sana kwaajili ya kununulia vitu
vyenye thamani kubwa sana na pengine vya kifahari na thamani maradufu ya
vilivyopo sasa kama magari na majumba ya kifahari.
Umaarufu wake
umezidi kuongezeka baada ya kuanza kuishi maisha ya kitajiri na tabia yake ya
kupenda kuwanunulia wafanyakazi wenzake chakula wanapokuwa mikutanoni. Hupenda
pia kuchangia utajiri wake alioupata kutoka katika uwekezaji wa bitcoin na
wengine. Anamiliki kampuni nyingine kubwa ya fedha za kidigitali iitwayo AUGUR.
PIZZA STORY
Mnamo mwaka
2010 nchini FROLIDA mtaalam wa program LASZ HANYECZ alibembeleza kuuziwa pizza
2 kwa bitcoin 10,000 alizokuwa ametengeneza kupitia komputa ya nyumbani.
“Ilionekana
bei ya bicoin ingeshuka zaidi kwa siku za usoni hivyo niliona halikuwa wazo
baya kubadilishana na pizza”
Thamani ya
bitcoin 10,000 kwa sasa ni zaidi ya 400,572,430,000/= za kitanzania, na ndivyo
jina la utani la bitcoin lifahamikalo kama “pizza coin” yaani sarafu pizza lilivyopatikana.
Matukio ya
watu wakijutia kuhusu kuhisi kupoteza bahati zao adimu yameendelea kutokea
ambapo mwaka 2017 tweet moja iliyotumwa katika mtandao wa kijamii wa tweeter
tarehe 16 mwezi Mei mwaka 2011, ilionesha mtu mmoja alietumia jina la GREG
SCHOEN akijutia kwa kuuza bitcoin zake 1,700 kwa bei ya dola za kimarekani 0.3
(takribani 672/=) alizonunua kwa bei ya dola za kimarekani 0.6 (takribani
1,344/= za kitanzania kila moja) na baadae kupanda na kufikia dola za
kimarekani 8 (takriban 17,920/= za kitanzania kila moja) kwa kila sarafu. Hakika
anajutia mara nyingi zaidi kwa sasa ambapo leo hii angekuwa na utajiri wa zaidi
ya 68,097,313,100/= za kitanzania endapo angezitunza kwa miaka 6 tu.
Hizo ni baadhi ya story tu zinazovutia kuihusu
teknolojia hii inayoonekana kuwa changamoto kubwa na muujiza kwa watu wengi, mengi
yanazidi kutokea yakiwemo majuto na kubadili maisha ya wengi. Post ijayo tutaongelea
hatua zilizochukuliwa na nchi za afrika katika kuendana na mabadiliko haya ya
kiteknolojia.
No comments:
Post a Comment