Wiki chache zilizopita kampuni nyingi kubwa zilizokuwa zimekufa zimejizolea umaarufu kwa kutoa tangazo la kuzikubali sarafu digitali kama bitcoinkatika malipo.
Baadhi ya kampuni hizo ni kama LONG ISLAND ICED TEA CORP ambayo imebadilisha jina na kujiita LONG BLOCKCHAIN na siku hiyo hiyo mauzoyake kupanda kwa kasi na hatimae kukirudisha kiwanda hicho cha vinywaji katika ubora wake.
Kiwanda hicho kwa sasa kimetoa tamko kuwa kipo kwenye taratibu za kuachana na biashara hiyo ya vinywaji na kuanzisha biashara ya uchimbaji wa sarafudigitali kama bitcoin kwa siku za hivi karibuni.
Kampuni nyingine ifahamikayo kama AMERI HOLDINGS hisa zake zimepanda na kufikisha mauzo ya dola za kimarekani milioni 39 ambayo ni sawa naasilimia 71 ya hisa zote zilizopatikana kwa miaka ya nyuma. Msemaji mkuu wa Kampuni hiyo alikiambia kituo cha habari kilichopo nchini humo kuwaimeshuhudia ni jinsi gani dunia inavyozidi kubadilika na watu kuzidi kuvutiwa na teknolojia hii ya sarafu digitali. Pamoja na hayo, AMERI HOLDINGS haitabadilisha aina ya biashara kama zilivyonyingine bali itadumisha zaidi huduma hiyo.
Tukiachilia mbali kampuni hizo maarafu, wafanyabiashara wadogo pia wamekili kupanda kwa mauzo mara tu baada ya kuiongeza huduma ya kupokeamalipo kupitia sarafu digitali.
Mbali na mauzo, picha na stori za sehemu zao za kufanyia biashara zimefika mbali zaidi na kusambaa sehemu nyingi kuliko walivyotarajia.
“Unahisi dhumuni kuu ya kampuni hizi kukubali kutumia njia za malipo kupitia sarafu digitali ni ipi kuleta mvuto na kuitumia kama sehemu yakujitangaza au ni kutokana na kuifurahia huduma hii katika kufanya kazi zao mbali na masilahi?”
Andika maoni yako kupitia uwanja wa comment kwenyepost hii na tuijadili kwa pamoja.


No comments:
Post a Comment