Pages - Menu

Thursday, January 18, 2018

VENEZUELA YAAGIZA WATAALAM WA KUCHIMBA BITCOIN KUJIANDIKISHA ILI KUSAIDIA KUTENGENEZA SARAFU ZA NCHI HIYO.

Nchi ya Venezuela imefungua usajili maalum utakaofungwa tarehe 20 January mwaka huu wa kuandikisha wataalam wote wenye ujuzi wa kuchimba sarafudigitali kama bitcoin ili kuweza kujadiliana na kuanza hatua za uchimbaji wa sarafu za nchi hiyo.
Kulingana na maelezo ya raisi yaliyorushwa na vyombo vya habari vya nchi hiyo hadi sasa idadi ya watu waaliojiandikisha imefikia 860,811. Sarafu hiyoinayoenda kutengenezwa kwa kunakili na kuifanyia marekebisho teknolojia iliyotumika kubuni bitcoin itaenda kufahamika kwa jina la PETRO.


KAMPUNI ZAJIPATIA UMAARUFU KWA KUZIKUBALI SARAFU DIGITALI KATIKA MALIPO.


Wiki chache zilizopita kampuni nyingi kubwa zilizokuwa zimekufa zimejizolea umaarufu kwa kutoa tangazo la kuzikubali sarafu digitali kama bitcoinkatika malipo.
Baadhi ya kampuni hizo ni kama LONG ISLAND ICED TEA CORP ambayo imebadilisha jina na kujiita LONG BLOCKCHAIN na siku hiyo hiyo mauzoyake kupanda kwa kasi na hatimae kukirudisha kiwanda hicho cha vinywaji katika ubora wake.

Wednesday, January 17, 2018

BOBBY LEE ATABIRI MEMA KUHUSU CHINA NA SARAFU DIGITALI.

Kufuatiwa kuwepo kwa tetesi zinazosema kuwa serikali ya China imepanga kuzifungia kampuni zote zinazofanya biashara ya sarafu digitali nchini humo mara baada ya mwaka jana benki kuu ya nchi hiyo kuanzisha vikwazo juu ya kampuni zinazojishughulisha na uchimbaji wa sarafu digitali,, na ilianza kwa kutunga sheria ngumu zinazolenga kuzibana kampuni hizi.


Monday, January 15, 2018

NINI HATIMA YA RIPPLE?


Kulingana na sarafu hii kuendelea kuvutia wawekezaji wengi kutokana na lengo lake la kurahisisha mahamisho ya kifedha kwenye mashirika ya kibenki mbalimbali kwa gharama nafuu na haraka, tayari benki kama standard chartered na nyingine nyingi kubwa zipo mbioni kuanza kuitumia,  hii imepelekea idadi ya wawekezaji kuongezeka kadri siku zinavyokwenda.




HATIMAE UMOJA WA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI YAADHIMIA KUSHIRIKIANA KUTAFUTA NJIA SAHIHI YA KUENDANA NA TEKNOLOJIA YA SARAFU DIGITALI NDANI YA MWAKA 2018.


Kutokana hali inayoendelea kwenye nchi za Afrika mashariki ya kushuka kwa uchumi na kuendelea kuporomoka kwa thamani ya sarafu zake,umoja  wa Benki za Afrika mashariki unaoundwa na nchi 6 zimefikia lengo la kuanzisha sarafu yake ya kidigitali itakayotumika kati ya nchi hizo 6, japokuwa hali ya ongezeko la watumiaji wa sarafu digitali nyingine kama Bitcoin kuendelea kukua kwa kasi, hii imeonekana kuwa changamoto kubwa na kizuizi cha nchi hizi kuanzisha sarafu yake (EAC currency),

HATIMAE NJIA MPYA YA KULINDA USALAMA WA WAWEKEZAJI KATIKA SARAFU DIGITALI YAPATIKANA NCHINI GIBRALTAR....!


Sheria iliyopitishwa tarehe 1 January mwaka huu nchini Gibraltar inayozitaka kampuni zote zinazojihusisha na sarafu digitali hasa Bitcoin kuwa na leseni maalum za kiserikali kutoka mamlaka ya GFSC (Gibraltar Financial Service Commission).
The chief Minister of Gibraltar
Hon. Fabian Picardo

Saturday, January 13, 2018

ADA ZA KUHAMISHA BITCOIN KUPUNGUA

Baada ya kushuhudia gharama za mahamisho ya bitcoin yakipanda kwenye robo ya mwisho mwaka 2017, hatimaye zimeanza kushuka kwa mara nyingine. Leo tovuti ya Bitcoinfee.com imeonyesha wastani wa dola 15 kwa kila mahamisho ya bitcoin yaliyofanywa duniani.


Thursday, January 11, 2018

HATUA ZILIZOCHUKULIWA HADI SASA NA NCHI ZA AFRIKA KUHUSU SARAFU HIZI HASA BITCOIN.


KENYA NA AFRIKA YA MASHARIKI
Kenya ilijulikana kupitia Bitpesa (Tovutia inayoweza mteja kubadili bitcoin kuwa fedha na fedha kwa bitcoin) ambayo imesaidia nchi za afrika ya mashariki kuitumia sarafu ya bitcoin kwa

HISTORIA ZA MATAJIRI WAKUBWA DUNIANI WALIOWEKEZA KATIKA BITCOIN NA SARAFU ZA KIDIJITALI KWA UJUMLA.


WINK LEVOSS




Mapacha hawa walizaliwa mnamo tarehe 21 mwezi August 1981, wajasiliamali wakubwa wa biashara za internet (internet). Umaarufu wao ulianza mwaka 2014 mara baada ya kumshitaki Mark Zuckerberg (mmiliki wa mtandao wa kijamii wa facebook) madai ya kuwa aliiba wazo lao la mtandao wa kijamii unaounganisha watu. Walishinda kesi hiyo na kulipwa takribani dola milion 65 za kimarekani (takribani sh 139,750,000,000/= za kitanzania).

Wednesday, January 10, 2018

HISTORIA YA BITCOIN NA FEDHA DIGITALI KWA UJUMLA

Mnamo january 3 2009 bitcoin(sarafu digitali) ya kwanza iligunduliwa na mtaalamu wa kuunda programu mbalimbali za kompyuta na masuala ya kiuchumi aitwae SATOSHI NAKAMOTO.
Kabla Satoshi Nakamoto kutoweka kusikojulikana aliweka utambulisho wake wazi akijitaja kama raia wa wa japani mwenye umri wa takribani miaka 37. Utambulisho unaonekana kuwa sio sahihi kulingana na uwezo wake wa kuandika lugha ya kingereza kwa ufasaha na katika kuunda program iliyotumika kutengeneza bitcoin na tovuti ya bitcoin.org